MACHINGA WAMSHUKURU NA KUMUOMBEA RAIS DKT SAMIA

 


Na Enea Marco- Nifahamishe News

Machinga kutoka Mikoa mbalimbali Tanzania wamemshukuru na Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hassan kwa namna anavyozipa kipaumbele na kuzitatua changamoto za Wamachinga nchini 

Akizungumza kwenye kongamano la Machinga wa kariakoo la kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hassan na kuombea Amani katika Taifa letu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani Wenyekiti wa Machinga Tanzania Steven Lusinde amesema serikali imeweka Mazingira wezeshi kwa wao Kufanya Shughuli zao kwa amani 

Lusinde amesema wameamua kufanya kongamano hilo ili kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hadharani kwani amewafanyia Mambo mengi machinga na hawana la Kumlipa Zaidi ya Kumshukuru na Kumuunga Mkono katika ajenda za Maendeleo 

“Tutaendelea kufanya Makongamano haya Nchi nzima tutapita kila sehemu kueleza Mema Ambayo Rais wetu Mpendwa Dkt samia Ametufanyia alisema Lusinde.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya wilaya amesema serikali imetenga zaidi ya Bilioni 317 kwaajili ya Masoko huku akitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wafanyabiashara ,Mamalishe na Bodaboda Pamoja na Makundi mengine ya wajasiliamali kuwa Ulinzi na Usalama wa Biashara zao ni wa Uhakika 

Sekta ya Umachinga mbali ya Kutoa Ajira kwa makundi mbalimbali pia inachangia Karibu asilimia 40 ya Pato la Taifa ( GDP )


Chapisha Maoni

0 Maoni