ZAIDI YA KAMPUNI 50 ZASAJILIWA.NANENANE


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News

DODOMA

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa rai kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kutumia maonesho ya Nanenane vyema kufika katika banda hilo waweze kupata usajili wa  papo kwa papo kusajili alama za biashara na makampuni papo kwa papo.

Mbali na hilo Brela imeyataka makundi kufika katika banda hilo kuweza kupata elimu mbalimbali ikiwemo kupapata usajili wa hataza usajili wakampuni.

Hayo yamesemwa leo Agosti 6,2024 na Afisa Kumbukumbu BRELA Faridi Ally Hoza alipokuwa akizungumza na vyombo vyahabari katika Maonesho ya wakulima Nanenane jijini Dodoma.

Amesema wakulima na wafugaji wanatakiwa kusajili alama za makampuni, alama za biashara na leseni ili waweze kufanya shughuli zao kwa tija na ubora.

Amesema Brela katika maonesho hayo wamewezesha kutoa huduma za usajili wa ainazote kwa haraka na papo kwa papo pindi mteja anapohitaji huduma katika maonesho hayo.

Katika maonesho hayo  wameshasajili zaidi ya kampuni 50 ambao wamefika kupata huduma katika banda hilo.

Amesema mbali na maonesho hayo Brela wameshafikia watu wengi kwa kutoa elimu kwakutumia njiambalimbali ikiwemo kutaumia maonesho katika mikoa yote nchini.

Yahya Hassan mmmoja wa wateja walioweza kupata huduma katika banda hilo amesema amefika katika banda hilo kwa ajili kufatilia huduma ya kusajili kampuni yake na ameweza kufanikisha kupata huduma hiyo ndani ya muda mchache jambo ambalo limemshangaza.

Amesema amefurahia kupata huduma kwa haraka tofauti na alivyotegemea’

“Nawasihi wengine wenye uhitajiwa kusajili leseni au hataza waje katika banda hili watapata huduma kwa haraka” amesisitizaa

Chapisha Maoni

0 Maoni