TANZANIA NA HUNGARY YASAINI MIKATABA IKIWEMO TEKNOLOJIA UDHIBITI WA MAFURIKO


Na Pilly Kigome

SERIKALI ya Tanzania na Hungary zimesaini mkataba wa ushirikiano katika sekta ya maji utakaosaidia udhibiti wa mafuriko na maji taka ambao umekuwa changamoto.

Mbali na mkataba huo Hungary pia inatarajia kufanya uwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza ndege ndogo mkoani Morogoro.

Mikataba hiyo umesainiwa leo Machi 28, 2024 Jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba na Waziri wa Mambo nje na Biashara Hungary Peter Szijjarto.

“Tumefanya mazungumzo ya kiserikali ikiwemo ushirikiano wa kibiashara ikihusisha makongamano, hivyo nchi hizi mbili zitakuwa zinafanya ziara za kibiashara kwa sekta binafsi,” amesema Makamba

Vilevile wataweza kufanya ziara za kibiashara kupanua wigo hasa katika sekta ya utalii mbapo kuwepo kwa ndege ya na usafiri wa moja kwa moja kutoka Tanzania na Hungary ili watalii wapate urahisi wa kufika kwa wingi nchini.

Chapisha Maoni

0 Maoni