MENEJA MKUU WA KAMPUNI VELTEX HERBERT SWAI KATIKA VIWANJA


Na Pilly Kigome

DAR ES SALAAM

WATANZANIA wametakiwa kutumia fursa ya kuwezeshwa kupata matibabu ya afya kwa wale wanaohitaji kwenda nchi za nje kwa kutumia Wakala wa huduma ya afya Veltex kwa njia ya haraka na uhakika zaidi.

Akizunguma jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Meneja wa Kampuni ya Veltex, Herbert Swai amesema kwa kutumia kampuni hiyo Mtanzania ataweza kutafutiwa matibabu kwa njia ya haraka kwenda nchi za nje kama Uturuki, Uingereza, India, Afrika Kusini na nchi zingine kupatiwa matibabu kwa haraka na uhakika na kwa njiaya usalama.

Pia Veltex wanaitangaza Tanzania kwa kuwaalika wagonjwa kutoka nchi jirani kuja katika matibabu katika hospitali za Serikali ikiwemo Muhimbili na Jakaya Kikwete (JKCI) kuja kupata matibabu yao kwa haraka na uharaka na uhakika.

Amefafanua wanahakikisha wanasimamia utaratibu wa kukata tiketi, kupata Viza ya kuja nchini jinsi ya kuweza kupokelewa akifika nchini hata kama mgonjwa anayekuja ni mahututi ataweza kupokelewa kwa njia ya usalama kwa ambulance maalum na maafisa kutoka ndani ya kampuni hiyo.

Kuhakikisha wanasimamia malazi, kuandaa appointment ya kuonana na madaktari bobezi kwakusimamiwa na maafisa kutoka kampuni hiyo.

Amefafanua Veltex inaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii tiba kuitangaza Tanzania kuwa kama kitovu cha matibabu ya afya na kutangaza madaktari wetu bingwa waliopo nchini.

“Tayari tumeshahudumia zaidi ya wagonjwa ya 68 katika huduma hizo kwa kuimarisha afya za watu” amefafanua

Mkurugenzi Mtendaji wa Women Tapo, Lulu Nyapili amesema wanajikita kuelimisha wanawake wanaofanya shuhuli zao sokoni kuwaelimisha kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia, rushwa za ngono, kutambua haki za ardhi na jinsi ya kujikwamua kiuchumi.

MKURUGENZI WA WOMEN TAPO LULU NYAPILI KULIA AKISOMA HOTUBA KATIKA MAONESHO

Amesema taasisi hiyo imeanza na kuwafikia wanawake wa Jimbo la Ilala na wanajipambanua kuwafikia wanawake wa mkoa mzima wa Dar es Salaam.

Edna Mkono ni mwanamke aliyeinuliwa na Tapo hiyo kutoka Tabata kwa kuwezeshwa mtaji na kupata elimu mbalimbali za ujasiriamali alianza kupatiwa mtaji wa elfu 50 na kutokana na elimu aliyoipata sasa mtaji wake umekua na kufikia shilingi laki na nusu.

MMOJA WA MNUFAIKA WA WOMEN TAPO TABATA EDNA MKONO

“Naishukuru sana Tabata Tapo wameniinua walivyonipa mtaji nimeanza kuuza biashara ndogondogo kama karanga, tambi,mkachori na nyingine nyingi.

Mratibu wa Afya kwenye Jamii Dkt.Asha Mahita aliwataka wanawake kuangalia afya zao mara kwa mara kwani mwanamke ni afya

“Mwanamke thamini afya yako kwani afya yako ndio mtaji wako wanawake tuwekeze kwenye afya” amesema