WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI JANUARY MAKAMBA AKIŹUNGUMZA NA.WAANDISHI WA.HABARI
Na Pilly Kigome-
Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajia kuanza ziara nchini Uturuki yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Mbali na hilo ziara hiyo ina lengo la kujiimarisha kiuchumi, kisiasa na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Hayo yamesemwa leo Aprili 15 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano Afrika Mashariki, Januari Makamba alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Waziri Makamba amesema Rais Samia na ujumbe wake anatarajia kuwasili nchini Uturuki Aprili 17 mwaka huu kuanza ziara hiyo.
Amesema nchi ya Uturuki imeendelea kibiashara na kiuchumi ni kati ya nchi 20 za G20 duniani hivyo ziara hiyo Tanzania inatarajia kunufaika katika nyanja nyingi ikiwemo wa kibiashara
Ikiwemo na kuimarisha ziara ya kihistoria pamoja kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo na maeneo ya uwekezaji.
“Nchi yetu tunahitaji masoko, biashara, uwekezaji, teknolojia kutoka kule, kwani Uturuki kuna makampuni 15 makubwa hivyo tunahitaji uwekezaji ikiwemo katika elimu, uchumi na kwingineko” amefafanua Makamba
Aidha alieleza Tanzania inanufaika na kuuza bidhaa za mazao, vito na madini kupeleka nchini Uturuki, hiyo imefanya uchumi waTanzania kupanda kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na miaka sita iliyopita.
0 Maoni