DAR ES SALAAM
Na.Pilly Kigome
WAZIRI Mkuu Kasimu Majaliwa anatarajiwa kufungua kongamano lililoratibiwa na Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania TAHLISO.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jinini Dar es Salaam makao makuu ya JUMIKITA kuhusiana na maandalizi ya kongamano hilo la kihistoria Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Shaaban Matwebe amesema Kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili undishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo.
"Lengo la Kongamano hilo kuwaleta pamoja waandishi wa habari kujadiliana kwa pamoja juu ya uandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani". Amesema Matwebe.
Amesema pamoja na kuwaleta pamoja wadau wa sekta hiyo pia kongamano hilo litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuadhimisha miaka mitatu ya tangu kuanzishwa kwa jumuia hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa Kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500 Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na changamoto ili kiundeshaji wa mitandao hiyo.
Matebwe amebainisha pia kongamano hilo litatoka na mapendekeze ambayo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa (information economics) na uchumi wa taarifa (information economy) kwa ustawi wa nchi yetu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti waandishi wa habari wa mtandao huo wamesema amefurahia ujio wa kongamano hilo kwani litawaunganisha na kuwakutanisha kwa pamoja ikiwemo kubadikishana mawazo na kuongeza ujuzi.
0 Maoni