RC ALBERT CHALAMILA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI
DAR ES SALAAM
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Albert Chalamila amewataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazotolewa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii wanaodai uchaguzi utakuwa na vurugu jambo hilo si kweli na kuwahakikishia wananchi kuwa Dar es Salaam ni salama sana.
Hayo ameyasema leo Oktoba 27, 2025 katika mkutano wake na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Mh.Chalamila amesema wananchi wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kupigia kura na kufafanua mkoa huo una wapiga kura zaidi ya M.4.
Amesema Tume ya Huru ya Uchaguzi imeshakamilisha miundombinu mizuri kwa wananchi kufuatia zoezi hilo.
Mbali na hayo Chalamila amevionya vikundi vinavyotishia kuvuruga amani ya nchi na kubainisha vyombo vya dola viko macho muda wote.
"Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wake wanapata haki yao ya msingi ya kikatiba ya kupiga kura pasipo na kubabaishwa na mtu yoyote" amesema
Aidha amevitaka vyombo vya habari nchini kufanya kazi kwa weledi kuripoti kwa usahihi na kuacha upotoshaji kwakuwa wao ni mhimili mkubwa wa kuunganisha wananchi na Serikali yao.



0 Maoni