BALOZI FATMA KIKKIDES AHIMIZA AMANI KWA VIJANA

FATMA KIKKIDES BALOZI WA AMANI NCHINI


Mwandishi Wetu-Nifahamishe News

MRATIBU Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania(JMAT) pia Balozi wa Amani Taasisi ya Wanawake Nchini Korea Kusini Fatma Fredrick Kikkides amewataka vijana walinde amani ya nchi wasidanganyike kwa kufata mikumbo wa mitandaoni.

Kikkides ameyasema hayo katika mahojiano maalumu aliyoyafanya Oktoba 23,2024 na Televisheni ya Taifa TBC 2 .

Amewataka vijana walinde amani ya nchi iliyopo wasiipoteze wao ndio nguzo kwa kuwa na kundi kubwa la vijana ambayo ni nguvu kazi.

Alifafanua vijana wanatakiwa wajitambue na kutofata mikumbo ya wanaotaka kuharibu amani ya nchi kwa kufata wahuni wa vijiweni wanaotaka kuharibu amani ya nchi.

"Nawaomba vijana watambue amani inaanzia kwenye nafsi, nyumbani, ofisini hivyo ni lazima muilinde amani kwa kizazi kijacho msiangalie sasa hivi tu tulipeleke Taifa la amani" amesema Kikkides

Aidha amefafanua kuwa vijana wengi wana changamoto ya kukosa elimu ya kuijua amani na wengi wao kufata makundi mabaya kwa hasira za kukosa ajira nankuamua kufata mikumbo ya mitandaoni.

"Nawaomba vijana jitokezen8 kwa wingi mkapige kura kachagueni viongozi sahihi watakaolisogeza nchi mbele na msidanganyike na mitandao wanaohimiza kuichafua nchi" amesema Kikkides

Chapisha Maoni

0 Maoni