WILAYA 114 ZAUNGANISHWA NA MKONGO WA TAIFA




Na Pilly Kigome

DODOMA

WILAYA 114 kati ya 139 zilizopo Tanzania Bara zimeshaunganishwa na mkongo wa taifa na kufanya watanzania kupata uchumi wa kidigitali.

Hayo yamesemwa leo Agosti 4, 2025 na Afisa Masoko Kitengo cha Mkongo wa Taifa kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL) Robert Rwamaya alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika.maonesho ya Wakulima mkoani Dodoma.

Mkongo wa Taifa ni njia kuu za mawasiliano ambazo zinawezesha watoa huduma za mawasiliano nchini na Afrika Mashariki kati kuweza kuunganisha mawasiliano na mabara mingine.

Wakati huohuo Wakulima,wafugaji na wavuvi wametakiwa kukimbilia teknolojia wezeshi mpya ya kuhifadhi taarifa zitolewazo na Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL) zitakazowawezesha kuepukana na upotevu wa taarifa zao za nyuma katika kazi zao.

Kupitia huduma hizo makundi hayo yatawawezesha kupata mazingira sahihi ya kuhifadhi taarifa zao pindi wanapohitaji mapitio ya taarifa za nyuma.

Afisa Tehama (TTCL) Geophrey Mlewa ameeleza kuwa makundi hayo wataweza kunufaika na huduma hiyo ikiwemo kuhifadhi taarifa zao muhimu yaliyowapa tija kwa wakati husika wa kilimo, uvuvi au ufugaji na kuweza kuyahifadhi kupitia mifumo hiyo kwa matumizi ya baadae.


 


 


 

Chapisha Maoni

0 Maoni