DODOMA
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News
Wakulima wametakiwa kutumia mbegu zenye ubora zilizothibitishwa na kuwekewa lebo ya ubora ili kuleta tija katika kilimo bora kitakacholeta matokeo makubwa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu waTaasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania(TOSCI) Nyasebwa Chimagu alipokuwa akizungumza na vyombo vyahabari katika maonesho ya Wakulima Nanenane mkoani Dodoma.Chimagu amesema wakulima wanatakiwa wanunue mbegu bora ambazo zimethibitishwa kwa matumizi zenye nembo na lebo ya TOSCI nakuingiza namba za vocha *148*52 kuthibitisha ubora wa mbegu.
“Mkulima yoyote ahakikishe anaponunua mbegu ahakikishe ananunua mbegu zenye sifa na lebo hiyo na akinunua apewe risiti kinyumena hapo mbegu hizo ztakuwa hazina ubora” amefafanua
Amesema Matumizi ya mbegu bora yamezidi kuongezeka ambapo zaidi ya wakulima 3618 walifika banda la TOSCI kwenda kupata elimu kuhusiana na mbegu bora.
Aidha amefafanua mbegu bora inalipa na pia mbegu bora ni ajira hivyo Serikali ina mpango wa kutoa ruzuku ya mahindi kwa kuwa mahindi ni chanzo cha kipato na wakulima wataweza kujipatia kipato.
Wakulima 5156 tayari wameshasajiliwa kupata mbegu za ruzuku na wanaweza wakaenda kokote wakapata mbegu hizo.
“Tumeweza kutoa elimu kwa zaidi ya wakulima elfu tano, wakulima wameweza kununua mbegu kupitia maonesho hayo ya nanenane”
Aidha amefafanua baadhi ya majukumu ya TOSCI ni pamoja na kudhibiti mbegu kuanzia shambani hadi kufikia sokoni.
Vilevile amethibitisha kuwa TOSCI imepata Ithibati ya Kimataifa ya udhibiti wa ubora wa mbegu, kwa kuuza mbegu ndani na nje ya nchi.




0 Maoni