Na Mwandishi Wetu
DODOMA
NAIBU Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Mhe. Cosato Chumi aipongeza Wakala wa Nishati Vijijini(REA) namna ilivyotekeleza Miradi mbalimbali vijijini na kuleta tija kwa wananchi.
Agosti 7,2025 Mh. Chumi alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la REA katika maonesho ya Wakulima Nanenane
Amesema Miradi yote inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imekuwa na athari chanya kwenye maendeleo ya watu waishio vijijini.
“Nawapongeza REA kwa kazi nzuri na ufanisi katika kutekeleza Mradi wa Ujazilizi II (C) na Mradi wa Taa za Barabarani, Sisi Mafinga ni wanufaika wa Miradi ya REA.” Amefsfanua Mhe. Chumi.


0 Maoni