MALANGE AAHIDI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO MBURAHATI

 

BENEDICTO MALANGE AKIWA KATIKA OFISI YA KATA YA MBURAHATI

Na Mwandishi Wetu-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

Benedicto Joseph Malange Mgombea Udiwani Kata ya Mburahati kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ameahidi kumaliza kero ya maji na barabara pindi apatapo ridhaa ya kuchaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo.

Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam Agosti 27,2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurudisha fomu ya uteuzi ktika ofisi ya Kata.

Malange amesema atakwenda kuibadilisha kata hiyo kwa kuleta shughuli za maendeleo ndani ya kata hiyo katika mitaa yote kwa kasi kubwa kwa kusimamia sera ambazo chama kimemuelekeza.

“Nikipata ridhaa nitaanza na changamoto kubwa ambazo zipo ndani ya kata hii ambayo ni barabara na maji ikiwemo na uzibuaji wa mifereji, maji yapo lakini kuna mtaa mmoja wa National Housing kuna uhaba wa maji maji huwa hayatoki siku zote za juma nitaenda kurekebisha kero hiyo”. amefafanua

Aidha ametangaza na kuahidi kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha wanajua mapato na matumizi ili kuondoa minong’ono na migogoro kutoka kwa wakazi.



Chapisha Maoni

0 Maoni