Na Mwandishi Wetu- Nifahamishe News
DODOMA
GESI asilia imegundulika kuwa na faida kubwa katika makundi yote ikiwemo wakulima na wafugaji kuwarahisishia katika utendaji wao wa kazi katika kusafirisha mazao.
Katika vyanzo vya nishati safi wameigundua kuna vitu viwili na kuleta faida kubwa ikiwemo kuboresha afya na kuwawezesha wakulima na wafugaji kufanya kazi kwa ufanisi.
Hayo yamesemwa leo Agosti 7,2025 na Mkuruenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petrol(PURA), Mhandisi Charles Sangweni alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Maonesho ya Wakulima katika viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma.
Amesema sekta ya gesi asilia na sekta ya kilimo zinategemeana kwa karibu ambao sekta hizo zikifungamanishwa vizuri zitaongeza tija katika uchumi wa chini.
Amesema sekta hiyo inaweza ikatumika kuzalisha ammonia, kemikali ambayo hutumika kuzalisha mbolea za aina mbalimbali ikiwamo urea.
Vilevile matumizi ya gesi asilia kwenye magari yamesaidia kupunguza gharama za uendeshaji
Kwa kuwepo gesi asilia wana miradi mbalimbali katika vyombo vya kusafirishia hivyo inawarahisishia wakulima kusafirisha kubeba mazao yao kutoka mashambani kwenda sokoni na kupata faida kwa ufanisi.
“Gesi huiwezi kuikwepa kwenye kilimo kwakuwa teknolojia imeweza kufanya kuwezesha kukausha mazao” amefafanua

0 Maoni