BUNIFU ZINAZOFANYWA NA VETA UTEKELEZAJI DIRA YA TAIFA 2050


8Na Mwandishi Wetu-Nifahamishe News

DODOMA


MAMLAKA ya elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi VETA imetakiwa kuwekeza nguvu kwenye uzalishaji mkubwa wa vitu vinavyobuniwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi mapana ya wananchi kwenye Maeneo yao kwakuwa ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya Taifa ya mwaka 2050

Mwenyekiti wa Bodi  VETA  Prof. Sefuni Ernest Mchome ameyasema hayo alipotembea banda hilo katika maonesho ya Wakulima Nanenane mkoani Dodoma.

Prof.Mchome amesema VETA inajukumu la kuhakikisha watanzania wa makundi mbalimbali wanapata elimu na mafunzo ya ufundi stadi ili mafunzo hayo yawasaidie katika maisha yao ya kila siku

Ameongeza kuwa Veta imepiga hatua kubwa katika ubunifu mbalimbali ambao unaoneshwa kwenye maonesho, kama bunifu zinazotimia nishati ya umeme, maji na nishati ya jua, na vifaa mbalimbali vinavyowasaidia wakulima kuvuta na kumwagilia inayotumia gharama ndogo 

Amebainisha kuwa mwaka jana kulikua na bunifu wa kutumia mapanga ya kusukumwa na nguvu ya upepo lakini mwaka huu ubunifu umeongezeka wa kutumia nishati ya jua.

Amezitaja bunifu nyingine kuwa ni vifaa vya kutengeneza chakula cha kuku, samaki na mifugo kwa kuwa gharama yake ni ndogo na zinaweza kuleta manufaa katika shughuli zao

Chapisha Maoni

0 Maoni