Na Pilly Kigome-Nifahamishe News
MKURUGENZI Mtendaji wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Mwajuma Hamza ameendelea kusherehekea mafanikio makubwa ya wanawake na jitihada kubwa wazipatazo wanawake kupitia chemba hiyo kwa kushirikiana na taasisi rafiki kuleta mafanikio makubwa kwa wanawake wajasiamali nchini.
Hayo ameyasema leo Julai 5,2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Hamza amesema TWCC imekuja kubadilisha mafanikio ya wanawake wafanyabiashara wadogo katika kujiendeleza kibiashara katika kuvuka kulifikia soko la dunia.
Amesema TWCC inawasaidia wanawake kuhakikisha wanafahamu vizuri huduma zinazotolewa na benki rafiki ya CRDB na kuwashika mkono wajasiriamali wetu kupata mitaji na kuwajengea uwezo kwenda masoko ya kimataifa.
Amesema TWCC ina program twende sokoni Afrika iliyozinduliwa mwaka huu inafanya vizuri katika kuleta tija kwa wajasiriamali nchini.
Naye Mkuu wa Uendeshaji Idara ya Uwekezaji Taasisi ya CRDB Joycelean Makule amesema benki hiyo inajikita zaidi kutengeneza madaraja ya wafanyabiashara wadogo wanaoanza biashara ili waweze kukua na kutengeneza uchumi ulio bora na hatimae kuwa na familia zilizo bora.
Makule amewataka wanawake hao wa TWCC kuondoa uwoga kwa kupeleka bidhaa zao kwenye masoko ya kimataifa kwa kuhofia bidhaa zao kuwa hazihitajiki.
"Msiwe na hofu ya bidhaa kwakuwa bidhaa zenu ni nzuri na zina viwango vya hali ya juu, "Sisi kama CRDB Foundation tunahakikisha tutawawezesha wanawake ili muyafikie masoko ya dunia” amefafanua
Aidha amesema wanawawezesha kuwapa elimu kurasimisha biashara kwa wajasiriamali wachanga wachanga na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotokana katika kazi.
TWCC inashiriki kikamilifu maonesho ya 49 ya Biashara kwa kinua na kuwajenge wanawake uwezo wa kibiashara kuwakutanisha wajasiriamali kutangaza bidhaa zao.
0 Maoni