TPDC KINARA MAENDELEO ELIMU NISHATI SAFI MAONESHO SABASABAI


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News

DAR ES SALAAM


SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli na Gesi (TPDC) imeibuka kidedea kwa kupata mshindi wa Maendeleo na Elimu ya Nishati Safi,kwenye maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Kilwa Jijini Dar es salaam.

Akizungumza Julai 7,2025 na vyombo vya habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano TPDC Maria Mselemu amesema,tuzo hiyo imetokana na  juhudi na utendaji kazi mzuri wa shirika hilo.

Amesema kutokana na juhudi kubwa na ushirikiano mkubwa kutoka kwa watumishi wa shirika hilo katika utendaji ni siri ya mafanikio kufikia ushindi ambao wanaupata kila mwaka.

"Tuzo hii ni ya tano kwenye maonyesho haya ya Sabasaba,lakini kwetu kama TPDC ni kawaida kwani tumekuwa tukipata tuzo kwenye maeneo taofauti ikiwemo tuzo ya Mazingira,na kwingineko"amesema Mselemu.

" Nakuongeza kuwa,kwa upande wa tuzo hiyo ya Mazingira tuliipata kutokana na kutengeneza mikakati ya kuondoa hewa ukaa kwa tani laki moja kwenye matumizi ya Nishati Safi ya kupikia".Aidha amesema kuwa kutokana na kutumia nishati safi ambayo inawekwa kwenye magari na kupikia,Wataalamu wa shirika hilo kufanyakazi kwa umakini ni kichocheo cha kuifanya TPDC kuwa kinara hadi kupatata tuzo mbalimbali ambazo zimekua hamasa kubwa kwenye utendaji wa kazi zao.

Chapisha Maoni

0 Maoni