Na Pilly Kigome-Nifahamishe News
DAR ES SALAAM
NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria Jumanne Sagini amehimiza Watanzania wenye changamoto mbalimbali za kisheria kukimbilia banda la Katiba na Sheria katika Maonesho ya Sabasaba waweze kupatiwa msaada wa kisheria papo kwa papo.
Ameyasema hayo leo Julai 8, 2025 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari alipotembelea banda la Katiba na Sheria katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa.
Sagini amesema banda hilo limejipanga na timu ya wataalamu wa kisheria hivyo watanzania wenye changamoto mbalimbali za kisheria wakimbilie na kupatiwa msaada wa kisheria.
"Nawasihi wananchi waje kwenye banda hili wapatiwe msaada wa kisheria Serikali yetu ni rafiki wamewaletea huduma ulipo na kusikilizwa kwa usikivu na hatimae kupata msaada" amesema
Amesema huduma ya msaada wa kisheria unahitajika na watanzania wote hata wasiokuwa na changamoto waje kujifunza na kupata elimu zinazohusiana na sheria.
Aidha amefafanua tayari kwa watanzania waliojitokeza kufika katika banda hilo wengi wanakuja kulalamika masuala ya migogoro ya ardhri na wanahudumiwa na
Maafisa husika wakiwemo kupatiwa elimu jinsi ya kumiliki ardhi na kupewa hati.
"Elimu hii ya sheria ikitolewa kwa wingi kwa wananchi migogoro mingi itapungua katika jamii yetu" amesema




0 Maoni