NIT YAANZA RASMI KOZI YA URUBANI

MKUFUNZI WA URUBANI NIT ASHRAFA RAMADHANI AKITOA ELIMU WA.MMOJA WA MTEJA ALIYETEMBELE KATIKA BANDA LA NIT


Na Pilly Kigome


CHUO Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeanza rasmi kozi ya mafunzo ya urubani nchini kwa mwaka mpya wa masomo 2025/26 ulioanza Julai mwakahuu.

Hayo yamesemwa na Mkufunzi wa Urubani NIT, Ashrafa Ramadhani alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) .

Ramadhani amesema kuwa kozi hiyo imeanza na wanafunzi kumi kati yao wanawake wanne na wanaume sita.

Amefafanua Chuo hicho kimejipanga vyema kutengeneza marubani wabobezi na wataalamu wa anga ambao italeta tija kwa Taifa kwa ujumla.

Kozi hiyo ambayo ni mpya kutolewa katika chuo hicho ambao inapokea wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi inakaribisha wenye sifa wachangamkie fursa hiyo kwa kupata ujuzi kwa gharama nafuu ambapo awali walikuwa wakiipata nje ya nchi kusomea mafunzo hayo na walikuwa wakitumia gharama kubwa.

"NIT tumejipanga vyema kikamilifu watu wasiogope kuja kwa kudhani labda hatutaweza waondoe dhana hiyo kwa kuwa tuko walimu wa kutosha ambapo kwa sasa tuko walimu kumi chuoni hapa" amesema

Aidha amefafanua vigezo vya kujiunga na kozi hizo ni rafiki kuanzia miaka 17 na ikiwemo na afya ya macho na akili vinazingatiwa na kuoewa kipaumbele.

"Wito wetu kama NIT tunaomba watu wakiamini chuo kuna vifundishia kazi vya kisasa kuanzia chini ya anga hadi angani na kuna ndege mpya kwa ajili ya wanafunzi hao maalum kwenye mazoezi yao" amesema.

Kwaupande wake Afisa Uhusiano NIT, Juma Mandai amewataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwakuwa inakwenda kuzalisha ajira za kutosha nchini.

Amesema mbali na urubani pia chuo hicho kinazalisha wataalamu wa anga ikiwemo wale watakaoweza kutengeneza ndege na ufundi wa matengenezo ya ndege.

"Kozi hizi ni maalum na tayari kuna uhitaji mkubwa wa wataalamu hao waje NIT waweze kupata utaalamu na kujipatia ajira ambazo ndani na nje ya nchi" amesema Mandai



Chapisha Maoni

0 Maoni