KAMISHNA WA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA(DCEA) ÀRETAS LYIMO
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)imetangaza operesheni maalumu ya kupambana na dawa za kulevya kwa kutoa elimu nchi nzima kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuoni ili kuweza kumaliza tatizo la dawa za kulevya nchini.
Hayo yamesemwa leo Julai 5,2025 na Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Lyimo amesema kuwa hali ya urahibu hivi sasa nchini imepungua kwa asilimia kubwa na kuendelea watumiaji wa heroin na cocain imepungua hii imetokana na Serikali kuwachukua warahibu na kuwahudumia.
“Kwasasa hata ukienda katika vijiwe vile vya warahibu walioathirika na madawa hata ukienda katika vijiwe kwenye maeneo mbalimbali na stendi watumiaji wamepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na elimu zinazotolewa kwa wananchi” amesema Kamishna
Amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya(DCEA) amesisitiza kuwekeza nguvu zaidi kwa watu walioathirika na urahibu wa dawa za kulevya kwa kuwapatia huduma stahiki ikiwemo kuwarudisha katika maisha yao ya kawaida kwa kuwapatia elimu.Amesema lengo la Mamlaka kuwa katika maonesho ya Sabasaba ni pamoja na kuwapa wananchi elimu na kujua kuhusiana na dawa za kulevya na kutambua wanapokamatwa na dawa za kulevya sheria inasemaje kuhusiana na dawa za kulevya.
Aidha amefafanua Serikali inatoa matibabu bure kwa wale wote walioathirika na dawa za kulevya.
0 Maoni