CRDB BIMA YAJA KUWAKOMBOA WAKULIMA NA WAFUGAJI

AFISA MAUZO BIMA KANDA YA PWANI JUSTINA BYALUGA 

Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

KATIKA kuboresha maisha ya Watanzania wote nchini wawe katika furaha na maisha ya kujiamini muda wote katika shughuli zao za kilasiku za kujitafutia kipato CRDB BIMA imeboresha huduma zaidi kwa kuwafikia na kurahisha maisha ya kila mmoja.

Hayo yamesemwa leo Julai 4, 2025 na  Afisa Mauzo Bima Kanda ya Pwani Justina Byalugaba wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ndani ya Viwanja wa Sabasaba jijini Dar es Salam.

Byalugaba amesema kuwa mwaka huu CRDB Bima imekuja kuboresha mara dufu zaidi ya huduma zake kuendana na matakwa ya wateja.

Amefafanua moja ya maboresho ikiwemo kama ile uharaka wa masuala ya malipo ya madai endapo mteja akipata ajali ambayo gharama zake ni chini ya Sh.Mil 3 hawatahitaji nyaraka kutoka polisi na wataangalia kwa uharaka bila usumbufu na ucheleweshaji uliokuwa ukijitokeza awali.

"CRDB Bima tumejipanga na tumeboresha hiyo sasa endspo mteja atapata shoda ya aina hiyo ndani ya saa 24 malipo yake yamekamilika na ataendelea kufanya kazi zake kama kawaida" amefafanua 

Maboresho ya huduma za bima ni pamoja na kuja na bima ya mifugo ambayo inawalenga wafugaji wa mifugo kote Tanzania ikitoa kinga inayopatikana kupitia mawaka wa Bima wa CRDB.

Majanga yanayolindwa na bima za mifugo ni pamoja na ajali, kuanguka, kupigwa shoti na umeme, kifo kutokana na moto, moshi, radi, mafuriko, kimbunga, maporomoko ya udongo, nguvu za nyoka na wadudu.

Mengine ni magonjwa ya Epidemiki kichaa cha Mbuzi, Anthrax, matatizo ya kuzaliana, uchinjaji wa dharura, wizi pamoja na magonjwa yanayosababisha kifo kama saratani ya muda mrefu na Mastitis

CRDB BIMA ahadi yao kwa wafugaji ni kulinda wafugaji wa mifugo wa Tanzania, kuhakikisha usalama wa chakula kwa taifa pamoja na kuunga mkono ukuaji na maendeleo ya kilimo na ufugaji

Mbali na wafugaji CRDB BIMA inawajali kada zote ikiwemo  kilimo na kuendelea kutilia mkazo KIJANI BIMA kwaajili ya maendeleo ya wakulima wakubwa na wadogo nchini. 

Wakulima wataweza kuhudumiwa moja kwa moja  kwa mawakala kota nchini.

Chapisha Maoni

0 Maoni