Na.Mwandishi Wetu
KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa Jessica Mshama amesema Chama hicho kinajali sana uwezo wa Vijana katika uongozi ndio maana kinawaamini na kuwapa nafasi za juu za kiuongozi.
Mshama amesema ameonesha uthabiti wa CCM katika uongozi wake kwa kuitofaugisha na vyama vingine kutokana na kuwaamini Vijana katika nafasi mbalimbali za kiuongozi na kwamba ushindi wa CCM hautokani kwa bahati mbaya kwa sababu kimejenga zaidi kwa Vijana.
Kuhusu suala la Uchaguzi, amesema kuwa Viongozi wa Juu wa Jumuiya ya UVCCM wamekuwa wakiratibu Mikutano inayohusisha Ziara zao katika Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha Vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kujiandaa kupiga kura ifikapo Oktoba 2025.
Mshama aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Watangazi wa Kipindi cha Sentro cha Clouds Tv kilichofanyika 08 Julai 8, 2025 katika studio za Clouds Tv Jijini Dar es Salaam.
Vijana Tunasema
OKTOBA TUNATIKI ✅
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#TunazimaZoteTunawashaKijani
#OktobaTunatiki✅✅✅

0 Maoni