BAHARI NI RASILIMALI MUHIMU TUILINDE NA TUIDHIBITI -NAHODHA MANDIA

NAHODHA MUSSA MANDIA AKIWA KATIKA BANDA LA TASAC

Na Mwandishi Wetu- Nifahamishe News

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa Sekta ya Usafirishaji kwa njia ya maji inachangia kuchochea uchumi hivyo inahitaji kulindwa na kudhibitiwa kulinda rasilimali hiyo.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Meli Tanzania(TASAC) Nahodha Mussa Mandia wakati alipotembelea Banda hilo la  katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya jijini Dar es Salaam.

Nahodha Mandia  amesema kuwa njia ya Usafiri wa majini kinachoangaliwa ni usalama wa vyombo pamoja na mizigo inayoingia ndani pamoja na vyombo vidogo vya ndani vinavyotumia maziwa.

Amesema  kuwa katika usafiri wa bahari shehena kubwa zinazoingia ndio zinakwenda kuchochea uchumi wa nchi katika kuongeza pato la Taifa.

"Bodi tumejipanga katika kushauri katika kuona matokeo  yanaonekana katika kuendelea kulinda usalama wa vyombo vya majini pamoja na abiria katika vyombo vidogo kwenye maziwa"amesema Mandia.

Amefafanua Serikali ya awamu ya Sita ya inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kuwekeza katika bandari mbalimbali na miradi hiyo itakuwa na matokeo mazuri katika katika kuendelea kuchochea maendelea kwa wananchi kwa uchumi wa mtu mmoja moja hadi taifa kwa ujumla .

Amesema katika Maonesho ya yanayoendelea wananchi watembelee Banda la TASAC kupata elimu kuhusu sekta ya usafiri wa majini.

Hata hivyo amesema wananchi  wanatumia vyombo vidogo katika usafiri waangalie usalama wao kwa kuwa na vifaa vya uokozi.

Chapisha Maoni

0 Maoni