Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM.
Kufuatia ufanyaji huo mzuri wa kazi kwa Wilaya hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ³TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa alimmwagia sifa Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kusema ana sifa zote za kuwa Mkuu wa Wilaya kutokana na utendaji wake mzuri na kujitoanna katika Wakuu wa.Wilaya wa Majiji anaongoza.
Waziri Mchengerwa amesema DC Mpogolo amenyooka katika uongozi wake anabadilibadilika sana, anafanya kazi kubwa sana kunsaidia Rais, anamsikiliza sana RC kwa kufuata maelekezo yake.
Amesema DC Mpogolo anaendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita kwa kuyashika makundi yote katika jamii yakiwemo bodaboda, mamalishe na makundi mengine mengi anayathamini.
DC Mpogolo amesema utendaji kazi wa pamoja na kuheshimiana katika kujenga umoja na mshikamano na kuleta tija kwa kazi za Serikali na kuwahudumia wananchi kwa manufaa ya maendeleo.
DC Mpogolo amesema Ilala itaendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya ili kuongeza mapato ya ndani katika halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.
Aidha ametoa ahadi ya kusimamia miradi yote ya maendeleo katika sekta mbalimbali ili iendane na thamani ya fedha zinazotolewa na serikali chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan.
Kuhusu suala la mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri ya jiji, Mpogolo ameeleza mikopo hiyo tayari imeanza kutolewa kwa mwananchi mmoja mmoja na vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu pamoja na kupatiwa elimu ili mikopo hiyo ikawe na faida kwa kuboresha biashara zao, kujikwamua kiuchumi na kurudisha kwa wakati ili vikundi vingine navyo vinufaike.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya na Meya wa jiji hilo Omary Kumbilamoto kwa kuendelea kuwa viungo muhimu kwa wabunge na madiwani kuhakikisha Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezeka.
0 Maoni