BAADHI YA TOYO AMBAZO ZINATAKIWA ZIRASIMISHWE ZINAZOFANYA SHUGHULU ZAKE MAENEO YA JIJI LA DAR ES SALAAM
Na Pilly Kigome
DAR ES SALAAM
WAMILIKI na madereva wa pikipiki za miguu mitatu Toyo za kubeba mizigo maarufu (maguta) zinayotumia nishati ya umeme wanaoendesha shughuli zao jijini Dar es Salaam wamepewa siku 30 kurasimilisha kusajili kuwa na leseni ya kuendesha vyombo hivyo.
Hayo yamesemwa leo Mei 21, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edrward Mpogolo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam alipokutana na wamiliki na madereva wanaoendesha vyombo hivyo.
Mpogolo amewataka waendesha maguta hayo kuwa na leseni maalum za udereva kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)ikiwemo na kuvikatia bima vyombo hivyo na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani na sheria za nchi.
Mpogolo amesema maadhimio hayo yana lengo la kuwaweka katika utaratibu mzuri kuendesha shughuli zao za kujiingizia kipato chao cha kila siku pasipo kubughudhiwa na mtu yeyote.
Amefafanua katika eneo la Kariakoo pekee kuna waendesha maguta zaidi ya 3500 ambao wanaendesha vyombo hivyo pasipo utaratibu maalum ikiwemo kukosa leseni, bima na vitambulisho vya kazi wakiwa kwenye shughuli hizo.
“Hivyo Halmashauri imekuja na utaratibu mzuri wamepokea maagizo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuliangalia kundi hilo, hivyo changamkieni fursa nendeni darasani mkasome na waliosoma mkasajili vyombo vyenu ili muweze kunufaika na fursa zilizopo” amesema DC Mpogolo
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salam, El-Huruma Mabelya amesema mpango huo wa kuwataka waendesha maguta waende darasani ikiwemo kurasimisha biashara zao ina lengo la kuwawekea utaratibu mzuri wa kuendana na fursa zilizopo nchini.
Ikiwemo kuondoa kero kwa wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo ambao wamekuwa wakiwalalamikia maguta hayo kuharibu utaratibu na kuleta msongamano mkubwa na kuziba barabara na kuleta bughudha kwa watumiaji waingiao eneo la Kariakoo.
“Tutakwenda kusimamia utaratibu na kwenda kuwapangia maeneo ya kuegesha vyombo hivyo na atakayekaidi sheria itafata mkondo wake, kwakuwa tunataka Kariakoo ibaki kuwa Soko la Kimataifa lenye mpangilio, usafi, usalama na hadhi iliyopo ” amefafanua Mabelya
Afisa Mfawidhi kutoka Mamlaka yaUdhibiti na Usafiri Ardhini(LATRA) Mkoa wa Dar es Salaam,Ngeleza Pateli amesema kufuatia maagizo hayo vyombo hivyo vyote vinatakiwa kwenda kupatiwa namba za usajili, mwendesha guta anatakiwa awe na leseni ili kutambulika kuwa ni chombo cha usafirishaji.
Kwa kupitia utaratibu huo kila mmoja atapata fursa ya kupatiwa maelekezo atumie njia zipi wakati wanaendesha shughuli zao za kujipatia rizki na kuondokana na utaratibu wa ukiukwaji wa sheria za matumizi ya sheria za usafirishaji.
Wakati huohuo baadhi ya madereva hao walisema wako tayari kufuata maelekezo hayo lakini waliomba waongezewe muda wakurasimilisha vyombo hivyo
0 Maoni