DC MPOGOLO AWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI KUDUMISHA AMANI NCHINI

MKUU WA WILAYA YA ILALA EDWARD MPOGOLO


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News

DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo awapongeza viongozi wa dini nchini kwa mchango wao mkubwa wa kusaidia kuliombea Taifa kwa dua mbalimbali na kuifanya nchi iwe na amani.

DC Mpogolo amesema uwepo wa viongozi hao unalifanya taifa liwe na amani na utulivu wakati wote kutokana na juhudi zao kubwa la kuiombea nchi na kumuombea Rais wa nchi.

“Hii ni ishara kubwa ya kuwa wanamuuunga mkono kwa asilimia zote kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha amani wan chi” amesema

Amesema bila viongozi hao wa dini nchi isingeweza kuwa na hali  ya amani iliyopo.

Aidha alimpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Amani, Shehe Alihad Salim kwa kuwa kiungo kikubwa kwa kuunganisha taasisi zote na kituo cha utamaduni cha Irani na kuja na sauti za Rehema kuleta amani Tanzania.

Pia alitangaza na kusema jiji la Dar es Salaam liko salama na vyombo vya ulinzi na usalama viko imara hivyo tutakwenda kwenye uchaguzi mkuu na amani na utulivu.


Chapisha Maoni

0 Maoni