DC MPOGOLO ASITISHA KIBALI UJENZI WA UZIO KIPAWA

Na Mwandishi Wetu-Nifahamishe News Blog


DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Ilala,  Edward Mpogolo, ametatua kero ya ukuta katika Mtaa wa Karakata, Kata ya Kipawa  Uwanja wa Ndege kwa kutoa zuio la ujenzi wa ukuta kwa kusitisha kibali hicho.

Kero ya ukuta uliokuwapplp9 unajengwa 0na mwekezaji na kuziba barabara inayotumiwa na wananchi wa eneo.
 
Ametoa maelekezo hayo alipotembelea kukagua eneo hilo lenye mgogoro ambalo lilikuwa linaleta kero kwa wakazi hao jijini Dar es Salaam.
DC Mpogolo amesema kupitia ofisi yake na Mkurugenzi wa Jiji wanakwenda kuangalia mchakato wa hati ya eneo hilo ulivyo patikana na upimaji ulivyo fanyika na kushauri kwa mamlaka zingine ziamue mgogoro huo.

Aidha amefafanua nia ya kuelekeza maelekezo hayo ni kutokana na  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoa maelekezo kutaka kuona watu wote nchini wanakaa kwa amani. 

“Pia sisi viongozi ambao ni wateule wake anataka tuishi na shida za watu. Ni lazima twende kwenye utatuzi. Namtaka Mkurugenzi hapa pasiendelee na ujenzi wowote kuziba barabara. njia ibaki kama ilivyo mpaka tutakapotoa  muafaka,”ameeleza Mpogolo.

Amesema amesikiliza maelezo ya pande zote mbili ikiwemo na kusikiliza wakazi wa eneo hilo hakuna eneo ambalo unaweza kusema upimaji wake ni upimaji wa pamoja au umeonesha barabara , kutokuwa na barabara, uchochoro au kuto kuwa na uchochoro,”amesema

Aidha maelezo wakazi wa muda mrefu wa eneo hilo àkiwemo Rehema Mvunye na Maulid Said walioanza kuishi eneo hilo tangu miaka ya 1980 walieleza ramani ya mwekezaji inaonekana kuingilia hadi maeneo  ya makazi, huku wakishangazwa na uhalali wa vibali vilivyotolewa licha ya Afisa mmoja wa Jiji la Dar es Salaam kudai kuwa eneo hilo lilipimwa rasmi.
 
Kesi ya Karakata ni kielelezo tosha cha jinsi falsafa ya 4R inavyoweza kutumika vitendo kutatua kero za wananchi na kuimarisha imani kati ya serikali na wananchi wake. Ni wito kwa viongozi wengine wa mamlaka za miji kote nchini kuiga mfano huu wa uongozi wa busara, uwazi, na utatuzi wa migogoro kwa ajili ya ustawi wa jamii.


Chapisha Maoni

0 Maoni