MTOKO WA PASAKA WAFANA, AMANII YAKUMBUSHWA



Na Mwandishi Wetu-Nifahamishe News


DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari amewataka Watanzania kuendelea kudumisha tunu ya taifa kwa kudumisha amani na Umoja uliopo nchini.

Ameyasema hayo leo April 20,2025 katika tamasha la Pasaka lililofanyika katika ukumbi wa SuperDome jijini Dar es Salaam.
Amesema katika nchi zilizobarikiwa tunuya amani Tanzania ni ya mfano hivyo Watanzania wanatakiwa wauenzi.

Amesema kwa kupitia matamasha haya ya dini yanawezesha kuwajenga kiimani kwakuwa Watanzania ni wamoja kwa dini zote.

Nae Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbi la Moto amesema kufuatia mgeni rasmi katika 'Mtoko wa Pasaka' kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Emmanuel Nchimbi ni ishara tosha kuwa chama hicho kiko karibu na wananchi wake wakiwemo wasanii.
Kwaupande wake muimbaji wa nyimbo za Injili Japhet Zabloon amesema matamasha haya ya dini ni mazuri kwani yanaenda kukutanisha watu wa kada zote na yana nguvu katika kuwaongezea watu imani na hofu na kuwa karibu na Mungu.

"Yanawasogeza watu karibu na Mungu na kujenga upendo kati ya mtu na mtu hususani katika kuzitumiza 4R kuelekea Uchaguzi Mkuu" amesema

Chapisha Maoni

0 Maoni