MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ALBERT CHALAMILA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI KATA YA SARANGA UBUNGO
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News
DAR ES SALAAM
RC Chalamila alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo apeleke fedha hizo ili ziweze kukamilisha ujenzi wa kituo hicho.
RC Chalamila ametoa agizo hilo leo April ,9,2025 katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo huku akisikikiza kero za wananchi Manispaa hiyo.
Alimtaka mkurugenzi huyo kupeleka fedha hizo wiki ijayo iki kutatua changamoto iliyopo ya kukosa kituo cha afya katika kata hiyo na kwenda umbali mrefu.
Wakati huohuo RC Chalamila amewasihi wananchi wa Mtaa wa Saranga kuwa wavumilivu wakati Serikali ikichukua hatua ya kutatua kero ya barabara ambayo wameikosa kwa muda mrefu nankuleta adha kubwa.
Vilevile amewataka wazazi na walezi kuwa waelewa kuwahudumia watoto wao vitu muhimu waendapo shuleni ikiwemo chakula na sare kwani hizo si jukumu la Serikali bali ni la kwao.
Awali alitembelea na kukagua mradi wa kusukuma maji Kibamba na kuweka jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Kituo cha Afya Mpiji Magoe na kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Goba kulangwa.
Akiwa katika kituo cha Afya Mpiji Magoe alimtaka fundi mwenyeji abomoe milango na kutoa frem za madirisha kwa kutokuridhishwa na ubora wa ujenzi huo.
0 Maoni