TASAC YAGUSA MAKUNDI MAALUM WAFUTU PAMOJA NA KUGAWA ZAWADI KWA WATOTO YATIMA


Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM

WAKALA wa Meli Tanzania(TASAC) imesema iko haja ya Mashirika, Taasisi na wadau wengine wa maendeleo ya jamii kuwaangalia kwa karibu na kuyasaidia  makundi maalum yasiyojiweza wasiojiweza ili kurudisha faraja na tabasamu kwa makundi hayo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi (TASAC) Nahodha Musa Mandia alipokuwa akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na shirika hilo.

Amesema makundi maalum yenye uhitaji yanatakiwa yaangaliwe kwa ukaribu kutokana na agizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.


“Leo tumeona tufuturu na makundi maalum ikiwemo hili la watoto yatima tumefuturu nao pamoja ili tuwakirimu kwani tumeusiwa na Mwenyezi Mungu tuwaangalie kwa karibu zaidi” amesema

Kwa upande wake Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam pia Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Tanzania, Shekhe Alihad Walid amesema kitendo kilichofanywa na TASAC ni kitendo cha uungwana na kinatakiwa kuigwa na mashirika mengine kuwafikia na kufuturu na kutoa zawadi kwa watoto yatima ni kitendo cha mfano.

“Tumeusiwa na Mungu kuwa tuwaangalie watoto yatima kwakuwa wanatamani na wao wawe kama wenzao kuwa na wazazi wao, hivyo sisi tuliobaki na wanaotuona ndio tuwe wazazi wao”amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea yatima cha Lady Fatima Kalekela Omari amesema kituo hicho kina jumla ya watoto 30 hadi ambacho kilianza na watoto saba toka kilipoanzishwa 2011.

Amesema wanawaomba matajiri na wamashirika mengine kuiga mfano wa TASAC kuwakirimu watoto hao na kuongeza wanatamani afadhiliwe nyumba kwakuwa hadi sasa bado wamepanga.

Chapisha Maoni

0 Maoni