NAIBU WAZIRI WA NISHATI JUDITH KAPINGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI WA NAMBA MPYA
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetekeleza agizo la Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko kuwataka kuanzisha namba ya bure ya huduma kwa wateja.
Leo Machi 12, 2025 Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amezindua namba hiyo mpya ya huduma kwa wateja (mchongo 180) itakayotumiwa na wateja bure bila malipo ili kupata huduma mbalimbali kupitia kituo cha miito ya simu cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Namba hiyo imekuja baada kuongeza wigo wa wapokeaji wa simu kutoka namba ya awali hadi 150 kwa awamu.
‘’Naomba niwahakikishie kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekusudia watanzania wapate umeme wa uhakika na kuongeza kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kuisimamia TANESCO na taasisi nyingine chini ya Wizara kuhakikisha sekta ndogo ya umeme inakuwa na kuleta maendeleo kwa Watanzania" amesema Kapinga
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Balozi Zuhura Bundala amesema mapinduzi kwenye utoaji huduma kwa wateja ni moja ya masuala ya kipaumbele ili kuchochea uchumi wa nchi na kuongeza kuwa shughuli za uchumi zinategemea sana uwepo wa umeme wa kutosha na uhakika.
Amesema bodi iko tayari kuhakikisha TANESCO inafanya kazi kwa bidii na jkutoa huduma bora kwa wateja ili kupunguza kero na changamoto za masuala mbalimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mh.Gissima-Nyamo Hanga amesena dunia ya sasa ni ya biashara na ushindani wa kibiashara unategemea uwepo wa huduma bora ya umeme na kutatua changamoto kwa wakati
Aidha amebainisha wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo uhamasishaji wa matumizi bora ya nishati safi kwa kutumia umeme.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati, bodi ya wakurugenzi ya TANESCO na wadau mbalimbali wa wa nishati na kushuhudiwa na wadau wa habari.







0 Maoni