Na Mwandishi Wetu-Nifahamishe News
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ubungo Dkt.Meshack Ole Sendeka wakati wa hafla ya Iftari kufuturu na watoto yatima iliyofanyika katika ukumbi wa Boxing Mafia KNOUT YA MAMA jijini Dar es Salaam.
Dkt.Olesendeka amesema jamii viongozi inatakiwa itambue uwepo wa yatima na watoto wenye mazingira magumu waweze kutimiza ndoto zao.
"Jukumu la kulea watoto yatima kuangalia usalama wao ni letu sote sisi ambao tuko hai" amesema
Nae Shamimu Shabani Mfinanga Katibu wa Elimu Malezi na Mazingira Tawi la Mabibo ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Uchumi, Fedha na Michezo Wilaya ya Ubungo muandaaji wa hafla hiyo amesema kwa sasa anajikita kuyafikia makundi maalum kuwasaidia ili kuweza kuwasaidia.
Mbali na kufuturisha wajane, walemavu, wastaafu pia ana ndoto za kuwasogeza kiuchumi na kuwatafutia makazi ya kudumu.
Amesema hivi sasa ana mpango wankufanya harambee ili fedha itakayopatikana aweze kuwanunulia kiwanja watoto hao wa kituo cha Madrasat Qatari kilichopo Kigogo wapate kujengewa makazi ya kudumu ambayo kwa sasa hawana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Madrasat Qamar Hassan Rajabu Mabruk ameomba watu wenye uwezo waweze kuwashika mkono kuwasaidia mahitaji muhimu kwenye malezi zikiwemo magodoro, nguo na vyakula ambavyo vinawasumbua.
Amesema kituo hicho kinakabiliwa nanchangamoto nyingi ikiwemo watoto kukosa magodoro ya kulalia ada za watoto ukosefu wa chakula ambapo kwa sasa hana msaada wowote kutoka kwa wafadhili anawasaidia mwenyewe.
Katika hafla hiyo pia kulifanywa dua maalum ya kumuombea dua RAIS Samia Suluhu Hassan pamoja na kuiombea nchi kuelekea uchaguzi mkuu
0 Maoni