MSEMAJI MKUU WA SERIKALI GERSON MSIGWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA HOTEL YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Mwandishi Wetu- Nifahamishe News
VIFO vya akina mama wajawazito vimepungua kutoka vifo 556 na kufikia vifo 104 na Serikali imeweka malengo hadi kufikia 2030 vipungue vifikie vifo 70.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali,Gerson Msigwa Machi Mosi,2025 mwaka huu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Amesema Serikali imefanya kazi kubwa kuleta mageuzi ya vifo hivyo katika kipindi cha miaka minne na kuondoa kabisa vifo hivyo kwasababu kuna uwekezaji mkubwa katika kukabiliana na vifo hivyo.
Kwa upande wa watoto chini ya miaka mitano amesema awali walikuwa wakifariki dunia watoto 67 katika watoto 1000 lakini kwasasa vimepungua na kufikia vifo 43.
Na Serikali imewekeza zaidi katika kukabiliana na vifo hivyo ikiwemo kutoa elimu kwa wamama wajawazito kuepukana na vifo hivyo ambavyo vingi vinatokana na changamoto za kuzaliwa nazo.
Amefafanua katika kipindi cha miaka minne cha Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 391.1 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Halmashauri nchi nzima, ikiwemo Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, na ukarabati wa Ofisi za Halmashauri.
Ikiwa na lengo la kuboresha huduma za afya za msingi na kumaliza changamoto za wananchi, ikiwemo ukosefu wa huduma za matibabu na vifaa tiba, na umbali mrefu wa kufuata huduma.
Katika eneo la huduma ya afya ya msingi Serikali ya imewekeza Tril.1 na Bilion 298 kuhakikisha watanzania wanapata dawa na kupata vifaa tiba vya kutosha.
Vilevile aliwataka wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia na kutunza majengo hayo, huku akionya kwamba kiongozi yeyote atakayekubainika kuwa na jengo lililoharibika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha amefafanua kwa upande wa sekta ya kilimo tayari Serikali imeshatumia Bilioni 225 kuanza ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji nchi nzima kuwawezesha wakulima .
1

0 Maoni