MSEMAJI MKUU WA SERIKALI GERSON MSIGWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI HABARI MKOANI KIBAHA PWANI
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
PWANI
MKOA wa Pwani unashika nafasi ya pili katika kuvutia wawekezaji katika sekta ya viwanda nchini.
Katika kipindi cha miaka minne kuanzia 2021 hadi 2025 mkoa wa Pwani umepokea miradi ya uwekezaji ipatayo 369 ambapo kati ya hiyo asilimia 67 ni miradi ya viwanda iliyogharimu mitaji dola za Marekani Billion 4.6 sawa na TSh.Tril.12.4 asilimia 61 ya mitaji hiyo inatokana na sekta ya viwanda na ikiwa ni mitaji ya dola za Marekani Bilion 2.8 sawa na TSh.Trillion 7.5.
Hayo yamesemwa leo Machi 16, 2025 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari eneo la Kwala Kibaha Mkoani Pwani.
Mradi huo ukikamilika utakuwa na viwanda vikubwa 200 na viwanda vidogo 300 vikiwemo viwanda vya kusindika vyakula, viwanda vya kutengeneza vifaa, dawa, ujenzi usindikizaji wa viatu, nguo na kemikali.
Amefafanua kukamilika kwa mradi huo kutaleta faida nyingi ikiwemo kutengeneza ajira za moja kwa moja zaidi ya laki moja na ambazo si za moja kwa moja zitafika laki tano.
Aidha amefafanua Mkoa huo umetengewa fedha kwa bajeti kwa kila wilaya kuna miradi ya maendeleo inaendelea mfano Bagamoyo ujenzi wa jengo la dharura wa Sh.Mil.300 unaendelea, ujenzi shule ya msingi, Kibaha ujenzi wa barabara zinaendelea, kwa upande wa Wilaya ya Kibiti Shule mpya ya Sekondari inajengwa, Kisarawe jengo la wagonjwa wa dharura, Mkuranga, mafia miradi ya maendeleo inaendelea kukamilishwa.
Pia amefafanua katika kipindi kifupi cha kuanzia Januari hadi Februari sekta ya viwanda imetengeneza miradi 52 ambapo ya watanzania ni 14 na ya wageni ni 33 ajira zilizotolewa ni 7,687 ndani ya kipindi hicho na kuonesha sekta hiyo inakwenda viuri.
Katika bandari ya kavu ya Kwala jumla ya makasha 800 yameshushwa na bandari hiyo ina uwezo wa kushusha makontena laki tatu(3) kwa mwaka na kwa siku ina uwezo wa kushusha makontena 823 sawa na asilimia 30 yanayoshushwa bandari ya Dar es Salaam.
“ Kwa takwimu hizi hapo tunakuwa tumepunguza presha katika bandari ya Dar es Salam kwa asilimia 30” amefafanua Msigwa
Wakati huohuo ametangaza kutolewa kwa vitambulisho vya kidigitali kwa waandishi wa habari ambapo wataingizwa kwenye mfumo kuwasaidia katika shughuli zao za kikazi kutambulika kwa haraka.
Kadi hiyo ya kidigitali itakuwa na taarifa za siri za muhusika na itawajengea heshima waandishi wa habari na kuondoa wimbi la makanjanja ambao wamevamia taalamu.
“Vitamblisho hivyo vitawatambulisha ndani na nje ya nchi, mtafanya kazi kwa weledi na mustakabali kwa tasnia yetu na maendeleo yetu pia” amesema.
0 Maoni