MIAKA 30 YA VETA YATASHEREHEKEWA KWA KISHINDO KUKARABATI MAJENGO YA UMMA

PROF.ADOLF MKENDA AKISISITIZA JAMBO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

KUELEKEA kusherehekea miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Ufundi Stadi(VETA)vyuo hivyo vitahakikisha vitaendelea kuzalisha wataalamu wapya watakaoweza kuleta ushindani ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo Machi 5, 2025 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo za Wizara ya Elimu jijini Dar es Salaam.

Prof. Mkenda amesema vyuo hivyo vimeendelea kuzalisha wataalamu mbalimbali kwa kada tofauti hivyo VETA kwa sasa inaendelea kujikita kuzalisha wataalamu wengi ambao wamezalishwa na vyuo hivyo kote nchini.

Amesema umuhimu wa elimu ya mafunzo ya ufundi ni kukuza ujuzi wa kiutendaji katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo na kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira na inahitaji ili kuongeza ufanisi katika uwekezaji.

Ikiwemo na kusaidia kukabiliana na changamoto za upungufu wa wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

Kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya VETA yanatarajiwa kufanyika kuanzia Machi 18 hadi 21, 2025 katika ukumbi wa JNICC na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Katika kuelekea kilele hicho shughuli mbalimbali zitafanywa kwa vitendo ikiwemo kutoa elimu kwa wingi kwa jamii, kukarabati majengo mbalimbali ya Umma yakiwemo ya Shule, Hospitali na mengine katika kuonesha mfano katika kazi zinazofanywa na vyuo hivyo.



Chapisha Maoni

0 Maoni