WAZIRI PROF.KABUDI AWATAKA WATANGAZAJI KUTOKUBANANGA LUGHA YA KISWAHILI

WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO PROF.PALAMAGAMBA KABUDI AKIZUNGUMZA SIKU YA REDIO DUNIANI KATIKA UKUMBI WA NEW GENERATION HALL MKOANI DODOMA

WASHIRIKI


Na Pilly Kigome- Nifahamishe News Blog

DODOMA.

WAZIRI wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi ameagiza watangazaji kuenzi na kufanya matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili katika utangazaji wa redio na uchapishaji.


Ameyasema hayo leo Februari 13, 2025 Mkoani Dodoma katika Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini ikiwemo na Maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Utangazaji na Uchapishaji.

Prof.Kabudi amesema, hivi sasa kumekuwa na upotoshaji mkubwa wa lugha ya kiswahili unaofanywa na watangazaji hasa redio na kukifanya kuwe na mmomonyoko na upotoshaji wa matumizi ya lugha hiyo.

Amesema matumizi ya neno H na A yanapotosha na kupoteza maana ya kile unachomaanisha hasa pale unapoiweka sehemu ambayo si sahihi akitolea mfano neno una na huna, ana na hana, uku na huku, na apa na hapa wengi hupotosha lugha kupitia maneno hayo.

Hivyo wamiliki wa vyombo vya habari wanatakiwa wafanye tathimini kubwa na kufatilia watangazaji na matumizi yao ya lugha kwani sasa kumekuwa na utofauti mkubwa sana ukilinganisha na awali kuwa mtangazaji ulikuwa uwe na sifa ya sauti na weledi ukilinganisha na sasa utangazaji unaweza kutangaza hata wasiokuwa na taaluma hiyo.

Aidha alitoa wito kwa wamikiki wa vyombo vya redio kuandaa vipindi vya kuielimisha jamii zaidi kwakuwa redio nyingi hivi sasa wamekuwa na vipindi vingi vya michezo kuliko vya kuielimisha jamii.

Kwa upande Wake Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari amesema mamlaka hiyo imejiwekea utaratibu wa kukutana na vyombo vyote vya habari, mara moja kwa mwaka.

Amesema lengo la kukutana ni kushauriana, kuelimishana pamoja na kutafuta majibu ya changamoto.

"Leo ni siku ya redio duniani. Kaulimbiu ni 'Redio na Mabadiliko ya tabia nchi'," amesema.

Anaeleza kuwa vyombo vya habari vinapaswa kutoa taarifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ili kuiwezesha jamii kuchukua tahadhari zote zinazoendelea na mabadiliko hayo.


Chapisha Maoni

0 Maoni