CRDB, SANLAM WAJA NA MASHIRIKIANO KUWAFIKIA WATANZANIA WA HALI YACHINI

 


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News

DAR ES SALAAM

BENKI ya CRDB na mfuko wa Uwekezaji wa Sanlam umeingia makubaliano ya mashirikiano katika uwekezaji wenye lengo la kuwafikia na kuwawezesha kuwafikia wawekezaji wote nchini.

Uwekezaji huo hautabagua mfanyabishara mkubwa au mdogo, uwe mfanyakazi, mjasiriamali wote tunalazima  kujiwekea akiba mbalimbali kwa ajili ya kujiendeleza katika maisha ya kila siku.

Njia mojawapo ya kujisogeza kimaisha na kujiwekea akiba ni kufanya uwekezaji katika masoko ya hisa na kujiongezea kipato kwa kupata faida za siku, wiki, mwezi na mwaka hiyo utajiongezea kipato itategemea unafanya uwekezaji wa ukubwa gani.

Hapa nauelezea uwekezaji katika   mfuko kutoka Sanlam Pesa na ukawekeza na kujipatia faida lukuki na kujikuta unaongeza utajiri wako kwa kuwekeza katika mfuko huo.

Ummy Hafidh kutoka katika mfuko wa uwekezaji wa Sanlam anaelezea kuwa mfuko huo wa uwekezaji hukusanya fedha kutoka kwa wawekezaji mbalimbali ili kununua dhamana za fedha kama vile dhamana za kiserikali za muda mfupi, hati fungani za Serikali, amana za Benki na hati fungani za kampuni.

Lengo kuu la mfuko huo ni kulinda mtaji na kupata mapato mazuri kwa muwekezaji ili mradi afikie malengo yake aliyojiwekea ya kila siku katika maisha yake ambapo ataweza kuhesabiwa  riba kila siku na kuongezewa faida kila mwezi.

Ameelezea kuwa mfuko huo anawekeza  mtu wa aina yoyote ambae anayehitaji kutimiza malengo yake na unawagusa watu wa kada zote wenye lengo la kumfanya kila mtanzania atimize ndoto zake kupitia mfuko huo, ambapo  mtu ana uwezo wa kuwekeza kuanzia shilingi elfu kumi ya kitanzania.

Tumeona hivi karibuni  mfuko huo ambao unaingia nchini umekwenda kuingia makubaliano ya mashirkiano na Benki ya CRDB kuweka mashirikiano ya kimkakati na kuchochea na kuimarisha kuongezeka kwa idadi ya masoko  na kuwaongezea fursa zaidi wananchi hasa wadogowadogo.

Makubaliano hayo ya uwekezaji yatakwenda kupanua  wigo kwa wawekezaji wa kitanzania na kuwawekea urahisi kuwaingizia faida lukuki kuanzia asilimia kumi na kuendelea.

Pia itakuwa suluhisho kwa watanzania kuchukua fursa na kuwekeza ikiwemo kuongeza mtitiririko kwa fedha za kigeni nchini.

Afisa Mkuu wa Fedha kutoka CRDB Fredrick Nshekanabo alifafanua kwa kina mashirikiano hayo yataleta tija ushiriki wa watanzania katika uwekezaji fedha hapa nchini kwa kupitia masoko ya mtaji na dhamana.


Utaleta manufaa makubwa kwa wananchi na jamii kwa ujumla kwakuwa Benki hiyo ya CRDB itakuwa wakala mkuu katika kuwawezesha watanzania wale ambao kwa njia ya kawaida wanakuwa hawawezi kufanya uwekezaji mkubwa na kuwarahisishia kuwekeza katika njia za kupitia miundombinu katika bidhaa za kidijitali  wawekeze katika masoko ya mitaji.

Hivyo kwa kupitia mashirikiano hayo hasa yana lengo la kuwafikia watanzania wapate huduma na fursa na ushiriki katika uwekezaji kupitia soko la mtaji na kuchochea ujumuishi wa fedha kiuchumi, kuimarisha masoko ya dhamana kuongeza uwekekezaji katika makundi mbalimbali ya wateja yakiwemo wale wadogowadogo.

Pia kuhamasisha watanzania waweke akiba katika soko la uwekezaji ambao hawapati nafasi ya kushiriki hasa makundi maalumu wakiwemo vijana,wanawake na wajasiriamali wadogowadogo.

“Tunakwenda kuwabadilisha watanzania wote ambapo uwekezaji huu hautamuacha mtu kwa ubaguzi wa uwezo hasa makundi maalum” alifafanua



 


Chapisha Maoni

0 Maoni