DAR ES SALAAM
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News
MVUA kubwa zinatarajiwa kunyesha katika maeneo yatakayopata mvua za wastani hadi juu ya wastani katika kipindi cha mvua za masiki zitakazoanza mwezi Machi hadi Mei mwakahuu.
Hayo yamesemwa leo Januari 23,2025 jijini Dar esSalaam na Kaimu Mkurugenzi (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a wakati akitoa taarifa ya muelekeo wa mvua za masika mbele ya vyombo vya habari.
Amesema mvua za masika zitakazoanza Machi hadi Mei zitakuwa za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi Nyanda za juu Kaskazini Mashariki pamoja na Mashariki mwa mikoa ya Mara na Simiyu.
Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini, Kaskazini mwa mikoa ya Kigoma na Ukanda wa Ziwa Victoria katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga.
Amesema vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi hivyo kusababisha uharibifu wa miundombinu, mazingira,mlipuko wa magonjwa pamoja na upotevu wa mali na maisha.

0 Maoni