USHINDI CCM "TULIJIPANGA NA UCHAGUZI" CPA MAKALA

KATIBU UENEZI, ITIKADI CCM CPA.AMOSI MAKALLA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News

DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Mapinduzi imezitaja sababu za kuibuka kidedea katika matokeo ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa ikiwemo maandalizi  mazuri ya kampeni, uratibu mzuri , Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, ikiwemo na migogoro iliyokuwa kwa wapinzani.

Sababu ya jumla ni wananchi kuridhika na na kazi inayofanywa na Serikali ya CCM ndani ya mitaa mbalimbali kujionea kwa macho  kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Uenezi,Itikadi na Mafunzo, CPA Amos Makalla alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo za CCM.

CPA. Makalla amesema ushindi wao wa asilimia 99 umetokana na kuandaa wagombea makini kuanzia ngazi ya shina.

“Tumeshinda wenyeviti kwa jumla ya mitaa 4,213 sawa na asilimia 98.83” amesema

Mbali na hilo CPA Makalla aliwashukuru Watanzania kwa kushiriki uchaguzi na kukipa ushindi mnono na kuahidi chama kitaendelea kuwatumikia wananchi wake kwa kusimamia ilani za chama.
“Kuna wanaodhani Demokrasiaya kweli ni hadi CCM ianguke ndipo waridhike si kweli demokrasia ya kweli sio lazima CCM ianguke, wanaopotosha waache kupotosha” amefafanua

Awali jana Novemba 28, 2024 Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa alitangaza matokeo na kubainisha CCM ilishinda kwa nafasi za vijiji 12,150 kati ya nafasi 12,280 na katika nafasi za uenyekiti wa vitongoji ilishinda kwa nafasi 62,728 kati ya nafasi 63,886 na huku CHADEMA ikiwa imepata viti 97 sawa na asilimia 0.79 katika uchaguzi huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni