DAR ES SALAAM
Na Mwandishi Wetu- Nifahamishe News Blog
ASASI ya Kimataifa inayohamasisha uwazi na uwajibikaji katika rasilimali madini, mafuta na gesi asilia tayari imeshatoa ripoti 14 za taarifa takwimu za kodi na mapato.
Hayo yamesemwa na Afisa Usimamizi wa Fedha (TEIT) Anastasia Ryoba alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Darnes Salaam katika mkutano wa 6 wa Kimataifa wa Uwekezaji katika sekta ya madini.
Ryoba amesema katika mkutano huo wamekuja kutoa elimu zaidi kwa wawekezaji na wananchi ili waweze kuijua zaidi kazi zifanyazwo na TEIT.
Amesema taarifa hizo wanazitoa kilamwaka wanahakikisha zinawafikia wananchi katika kuboresha ushilikishwaji Watanzania katika maendeleo ya jamii.
"Tuko hapa kutoa elimu kuhusiana na TEIT tunaomba washiriki watembelee banda letu kuja kupata elimu zaidi kuhusiana na shughuli tuzifanyazo" amesema Ryoba



0 Maoni