TCAA YAIBUKA MSHINDI WA TATU KWENYE MAMLAKA ZA UDHIBITI TUZO ZA NBAA

 


Na Mwandishi Wetu-Nifahamishe News


DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeibuka mshindi wa tatu kwa upande wa Mamlaka za Udhibiti katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2023 kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA).

Tuzo hiyo imetolewa leo Novemba 29,2024 katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. 

Katika tuzo hizo Mshindi wa kwanza amekuwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeibuka mshindi wa pili.

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uongozaji Ndege katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Flora Alphonce ameongoza ujumbe wa TCAA katika upokeaji wa tuzo hiyo.

Alphonce amesema wanaishukuru NBAA kwa kuwapa ushindi huo kwani unadhihirisha huduma bora wanazotoa nchini.



Chapisha Maoni

0 Maoni