SEKTA YA MADINI INAONGEZA PATO LA TAIFA - MAJALIWA



DAR ES SALAAM

Na Pilly Kigome- Nifahamishe News 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo kwakuwa wanamchango mkubwa kwa kuliongezea pato Taifa.

Tayari wameshawapatia na kuwawezesha kuwapa maeneo wachimbaji wadowadogo 350 pamoja na kuwapeleka wachimbaji zaidi ya 50 nchini China kwaajili ya kujifunza utalamu mbalimbali katika sekta ya madini ikiwemo na  kujifunza utafutaji wa soko la madini .

Ameyasema hayo leo Novemba 19, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa madini na uwekezaji Tanzania iliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC).

Amesema mkutano huo utawezesha kuimarisha ushirikiano mkubwa na kuongeza thamani ya madini na kuleta ustawi unaozunguka sekta ya madini.

Nae Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema kutokana na mchango mkubwa unaoletwa na sekta ya madini na Serikali kuìongezea bajeti wanakwenda kujenga maabara kubwa na ya kisasa mkoani Dodoma na kwenda kuwajengea uwezo  wataalamu wa GST.

Pia Serikali inajipanga kununua usafiri wa  Helikopta kwa kila Wilaya ili kuwezesha kufanya utafiti wa kina  katika sekta ya madini ambapo sasa wameshafanya utafiti wa urefu kwa asilimia 16 ambapo Tanzania nzima ina urefu wa Kilomita za mraba 945,000 sawa na hekari Mil.233.

Kwaupandewake Makamu wa Ŕais FEMATA ameiomba Serikali kuwapatia mashine za kuchimbia kujua miamba kila wilaya ambapo kwa sasa ziko 10.

Mbali na hilo aliiomba serikali wachimbaji wadogo wapate ruzuku ili kuongeza tija na hiyo italeta tija na kuongeza zaidi pato la Taifa.

Pia kuomba kuwe na leseni maalum kwa wachimbajì wadogo.



Chapisha Maoni

0 Maoni