DAR ES SAAĹAM
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
WAANDISHI wa habari zaidi ya 250 tayari wameshawasilisha kazi zao kutoka mikoa 23 kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards zinazotarajiwa kuhitimika Novemba mwaka huu.
Hayo ameyasema leo Oktoba 24, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji (TAMWA) Dkt.Rose Reuben alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari.
Reuben amesema Samia Kalamu Awards ni fursa muhimu kwa wanahabari kuonesha mchango wao katika maendeleo ya nchi na kuongeza ufanisi katika tasnia ya habari.
Amesema tuzo hizo zinalenga kuendeleza uandishi unaozingatia maadili, weledi na uzalendo kwakuwa mashindano hayo adhimu yatashirikisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji kura utakaoanza Novemba 8 2024.
Mashindano hayo yameandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania(TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya MawasilianoTanzania(TCRA)
Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Jabiri Bakari amesema kuwa muda wa kuwasilisha maombi umeongezwa hadi Oktoba 30 kutokana na changamoto za kiufundi, ikiwemo kushindwa kupandisha kazi mitandaoni na changamoto nyingine ambapo awali mwisho wa kuwasilisha maombi ilikuwa Oktoba 26.
Tuzo hizo zitatolewa kwa wanahabari wa Kitanzania zikiwa na lengo la kuhamasisha kukuza na kupanua wigo wa uandishi, utangazajina uchapishaji wa maudhui ya ndani kupitia vyombo vya habari vya asili na mitandaoni.



0 Maoni