MWALIMU WA MADRASA MATATANI TUHUMA ZA UBAKAJI


Na Mwandishi Wetu-Nifahamishe News Blog

KAGERA

JESHI la Polisi mkoani Kagera limemkamata na kumfikisha mahakamani Haruna Ayubu Rubai, mwenye umri wa miaka 63, ambaye ni Mwalimu wa dini ya Kiislamu na Daktari wa viungo anayemiliki kituo cha mazoezi ya viungo mjini Bukoba, kwa tuhuma za ubakaji wa watoto.

Rubai anatuhumiwa kutenda kosa hili mnamo Oktoba 19, mwaka huu, majira ya saa saba mchana, katika kituo chake kilichopo Kata ya Miembeni, Tarafa ya Rwamishenye, Manispaa ya B

Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, mmoja wa waathirika ni mtoto mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa mtuhumiwa huyo katika madrasa. Mtoto huyu alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kagera kwa matibabu, ambapo hali yake inaripotiwa kuwa inaendelea kuimarika.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mnamo Oktoba 22, 2024 majira ya saa nane mchana, mzazi Rayana Issack aligundua kuwa watoto wake wawili wamebakwa. Baada ya kufikishwa hospitalini, madaktari walithibitisha kuwa watoto hao wamefanyiwa ukatili huo, na walipoulizwa walimtaja Haruna Rubai kuwa ndiye aliyewafanyia vitendo hivyo.

Polisi pia wamebainisha kuwa mtuhumiwa Rubai alikuwa akitumia mbinu ya kuwasaidia familia zenye uhitaji kila Jumamosi. Katika mchakato huo, familia hizi zilikuwa zikituma watoto wao kuchukua mahitaji ofisini kwake, hali ambayo inaaminika ilimpa nafasi ya kutekeleza ukatili huu.

Mtuhumiwa Rubai amewekwa chini ya ulinzi mkali, na kesi yake inaendelea kuchunguzwa na vyombo vya usalama ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake. Jeshi la Polisi limewataka wazazi na walezi kuchukua tahadhari zaidi kuhusu usalama wa watoto wao

Chapisha Maoni

0 Maoni