TMA YATOA ANGALIZO KWA BAADHI YA SEKTA MSIMU MPYA WA MVÙA ZA VULI

DAR ES SALAAM

Na Pilly Kigome-Nifahamishe News

KUFUATIA mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo utakaoanza mwezi Oktoba hadi Disemba athari chache zinaweza zikajitokeza katika baadhi ya maeneo hivyo wadau wa kiuchumi na kijamii wanashauriwa kupanga na kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia taarifa mahususi za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka.

Kufuatia msimu huo baadhi ya sekta ikiwemo Kilimo na Chakula kutajitokeza upungufu wa unyevunyevu katika udongo unaotarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi yanayopata mvua za Vuli hususani maeneo ya nyanda za Juu Kaskazini Mashariki na Ukanda wa Pwani ya Kaskazini ambapo hali hii inatarajiwa kuathiri ukuaji wa mazao ikiwemo kuongezeka kwa wadudu katika kipindi na kupelekea kuathiri uzalishaji wa mazao.

Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA)Dk. Ladislaus Chang’a alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa mwelekeo wa mvua za msimu wa vuli katika kipindi hicho.

Chang’a amesema kuwa katika Sekta ya mifugo na uvuvi mvua hizo chache zinazotarajiwa kunyesha zinaweza kuathiri upatikanaji wa maji na miwasho kwaajili ya mifugo na chakula kwaajili ya samaki ikaathiri uzalishaji wa mifugo, mazao ya mifugo na samaki ikiwemo na uwepo magonjwa yanayoenezwa na kupe na wadudu warukao yanatarajiwa kupungua.

Amebainisha katika Sekta ya Utalii na Wanyamapori zitapekekea uwepo wa upungufu wa chakula na hivyo kusababisha migogoro kati ya jamii na wanyamapori kutokana na upungufu wa rasilimali, magonjwa ya wanyamapori yanayotokana na upungufu upungufu wa mvua yanaweza kutokea na kutapelekea kusambaa kutoka kwa wanyamapori kwenda kwa binadamu.

Kwa upande wa sekta ya Nishati na Madini katika kipindi hicho kunatarajiwa kupungua kwa maji katika mito, mabwawa na kupelekea kupungua kwa upatikanaji wa maji ka matumizi mbalimbali na kuwepo kwa upungufu wa uzalishaji wa sekta hiyo na kupelekea migogoro kati ya watumiaji wakubwa na wadogo.

Aidha katika sekta ya afya hali ya upungufu wa upatikanaji wa maji safi na salama kunaweza kujitokeza na kusababisha magonjwa ya mlipuko kama vile magonjwa ya ngozi kipindupindu na homa za matumbo, changamoto za kupumua na magonjwa yanayohusiana na joto kali.

Katika Sekta Binafsi shughuli za kibiashara zinazohusiana na hali ya hewa zinaweza kuathirika kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji kutokana na matumizi makubwa ya nishati uhifadhi wa mazao tete na bidhaa. Ukosefu wa mvua chini wa wastani zinaweza kuathri kwa ubora wa miti ya nguzo na mbao.

“Hivyo kutokana mwelekeo huo tarajiwa tunaiomba wananchi na sekta zote kuchukua tahadhari na ushauri tulioutoa” amesema Chang’a

Chapisha Maoni

0 Maoni