NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI SALAMA HAINA MADHARA-REA


MKURUGENZI MKUU REA ENG.HASSAN SAIDY AKIMKABIDHI JIKO LA GESI MTEJA
                   

Na Pilly Kigome-Nifahamishe News                                                  DODOMA                                 

WATANZANIA wametolewa hofu na wasiwawasi juu kupatikana kwa majanga katika matumizi ya nishati safi ya kupikia kwani Teknolojia iliyotumika kuweka mifumo katika nishati hiyo kupatikana kwa majanga ya moto ni mdogo kuliko zile nishati za zamani.

Mbali na hilo watanzania wametakiwa kuachana na upotoshaji juu matumizi ya nishati safi ya kupikia inaondoa radha ya chakula kuwa jambo hilo halina ukweli.

Hayo yamesemwa leo Agosti 8,2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati na Vijijini(REA)Eng.Hassan Saidy alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema Watanzania wanatakiwa wabadilike kuendena na mabadiliko ya kukua kwa teknolojia na kasi ya maendeleo yanayopatikana nchini.

Hivyo amewaasa watanzania kuachana na matumizi ya nishati chafu kwani mataumizi ya nishati hiyo ina madhara kubwa kiafya aktika mwili wa binadamu.

Amesema hivi sasa REA inafanya majukumu makubwa katika kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya nishtati hiyo kuwafikia wananchi wa vijijini kwa kushirikiana na vyombo vya habari na wadau wengine.

Amesema tayari tumeshaanza kusambaza majiko banifu na mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku ya serikali ili kusaidia wananchi kueneza nishati hiyo kwa gharama nafuu ili kila mwananchi aweze kunufaika na nishati hiyo.

“Ninawaasa wananchi wasiogope matumizi ya nishati safi kwani inapatikana kwa gharama nafuu, hivyo waachane na kuingia maporini kutafuta kuni kwani kuna madhara makubwa ya kukutana na wanyama na madhara mengine kuharibu afya kwa moshi utokanao na kuni” amesema

Katika banda hilo tumeshuhudia wananchi mbalimbali wamekuja kununua bidhaa mbalimbali ikiwemo majiko ya gesi na majiko ya mikaa safi kwa REA imetoa punguzo kwa bidhaa hizo katika kipindi hiki cha Sikukuu za nanenane.

Chapisha Maoni

0 Maoni