FCC YAWATAKA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUTUMIA BIDHAA ZENYE UBORA

MKURUGENZI MKUU WA FCC WILLIUM URIO

Na Pilly Kigome- Nifahamishè News Blog 

TUME ya Taifa ya Ushindani (FCC) imewataka wakulima wafugaji na wavuvi kutumia pembejeo zenye ubora ili waweze kupata mazao yenye ubora.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu (FCC) William Urio alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Maonesho ya wakulima na wafugaji Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma. 

Urio ameyataka makundi hayo kutumia maonesho hayo vyema kufika katika banda hilo kujifunza namna bora ya Tume ya Ushindani inavyofanya kazi hasa katika suala zima la kumlinda mlaji. Amesema Tume ya Ushindani ndicho chombo kinachoshughulikia masuala ya ushindani wa kibiashara pia ina jukumu muhimu la kutoa ushauri kwa kampuni zinazoshindana katika soko ikiwemo kujitambulisha kwa Soko, kulijua soko na mahitaji ya wateja.
Aidha amefafanua FCC ina jukumu la kuhakikisha mfanya biashara anatambua nafasi yake katika soko ili kuboresha bidhaa na upekee ili kuwa na tija katika kujitofautisha kupitia bidhaa ili kutoa huduma bora kwa wateja. 

Pia aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha bidhaa zake zinakidhi viwango vya ubora vinavyotambulika kisheria kwani hicho ni kiungo muhimu katika ushindani.

"Kwenye kilimo kuna suala zima la pembejeo hivyo ni wakati sahihi wa wakulima kuja na kupata elimu ya ufahamu ya pembejeo feki lakini pia kwa upande wa wavuvi wanahitaji elimu wanapataje nyavu sahihi bila kusahau vifungashio viwe venye kukidhi viwango, "Amesema


Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa,amewataka Wafanyabiashara na wakulima kwa ujumla kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata nafasi ya kuwachagua Viongozi wenye maono na fursa zinazowahusu. "Viongozi bora ni wale wenye mipango thabiti na mikakati ya maendeleo ya kilimo na kuweza kujumuisha mipango ya kuboresha miundombinu, masoko, na upatikanaji wa huduma za kilimo, " Amesema.

Chapisha Maoni

0 Maoni