Na Pilly Kigome-Nifhamishe News Blog
MAHAKAMA Kuu Kituo cha Usuluhishi Dar es Salaam kimepokea kesi zaidi ya 190 katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2024.
Hayo yamesemwa na Rahel Kangaga Hakimu Mkazi pia Msaidizi wa Sheria wa Jaji Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 Sabasaba.
Kangaga amesema kituo hicho kinapokea migogoro ihusuyo madai na mikataba zilizofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na zile zilizofunguliwa divisheni kuu ya ardhi.
Kangaga amefafanua kuwa migogoro hiyo inakwenda kituoni hapo kwa kuamriwa na Mahakama kufika hapo kwa usuluhishi.
Amefafanua migogoro inapofika katika Kituo hicho kunakuwa na faida nyingi ikiwemo kutoa faragha na hutunza siri wa mgogoro wa wadaawa, mchakato wa usuluhishi unaweza kubadilishwa ili kukidhi mahitaji ya wahusika ili kufikia maridhiano.
Hupunguza gharama kwa kila upande baina ya wadaawa na Mahakama, pamoja na kurudisha mahusiano mazuri baina ya wadaawa na kupunguza muda kusuluhisha mgogoro ukilinganisha nankesi za kawaida.
"Faida nyingine mgogoro unakamilika usuluhishi ndani ya siku 30 tu". amesema

0 Maoni