Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM
WILAYA 98 zimeunganishwa na mkongo wa taifa wa mawasiliano na wiialay 41 zilizobakia hadi kufikia mwezi Desemba mwakahuu zitakuwa zimeshaunganishwa katika miradi inayoendelea kwa sasa nchi nzima itakuwa imeunganishwa.
Hayo yamesemwa na Robert Lwamahe Afisa Masoko Kitengo cha Mkongo wa Taifa TTCL alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa Sabasaba katika banda la kampuni hiyo.
Lwamahe amesema kijografia nchi ya Tanzania imepakana na bahari ya Hindi hivyo inapokea mikongo ya baharini kimataifa ambayo inaleta huduma za mawasiliano nchini hapa Dar esSalaam na kuwa kiatovu cha mawasilinao AfrikaMasharikina Kati.
Tanzania imeweza kuunganisha huduma ya Faiba katika nchi ya Burundi kupitiampaka wa Kamanga na Manyovu, DRCkwa sasaikokatika mradi wa kuiunganisha na mkongo wa Faiba taifa ipokatikahatua za utekelezaji hadi ifikapo 2025, Zambia kupitia mpaka wa Tunduma,Malawi kupitia mpaka Kasumulu,Msumbiji kupitia mpaka Mtambaswala, Kenya imeungwa kupitia boda tatu Sarari, Namangana Horohoro.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni tanzu ya TTCL (T-PESA),Lulu Mkudde amesema watu zaidi ya 200 wamewasilisha maombi katika la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika maonesho hayo wanafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuandikisha watu ambao wanahitaji mtandao wa intaneti majumbani ama fiber.
“Tumepokea maombi mengi wateja wanahitaji huduma hii ambayo imeleta mapinduzi,yale malalamiko ya vifurushi vya intaneti kuisha haraka hapa hayapo,shirika limeleta huduma hii kumuwezesha mwananchi kutumia Intanet bila kikomo,”amesema.
Amesema kupitia mitandao wamefungua milango ya kidigitali kwakuweka mazingira wezeshi kwa wananchi katika kutumia huduma za Intaneti katika kutekeleza huduma mbalimbali kwa wananchi.

0 Maoni