WATANZANIA JITOKEZENI KUPIMA MAJI KUEPUKANA NA MATUMIZI YA MIONZI YATOKAYO CHINI YA ARDHI

 

PETER NGAMIRO MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO TAEC AKIZUNGUMZA WAANDISHI WA HABARI


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

WATANZANIA watakiwa kuwa makini kwakujali afya zao katika matumiaji sahihi ya maji ili kuepukana na magonjwa yatokanayo na matumizi ya mionzi yatokayo chini ya ardhi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Peter Ngamiro wakat akizungumza na vyombo vya habari katika maonesho ya 48 ya Tantrade yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amesema wananchi wanatakiwa kuwa makini matumizi ya maji hasa ya visima kwa kuyapima kuepukana na kutumia maji yenye viasili ya mionzi kwa kuepusha maradhi kwakuwa na uwepo wa mionzi asili kwenye udongo na mazingira kama vile madini ya urani.

Amewataka watanzania kuonyesha ushirkiano pindi waanapofikiwa kwani tumehiyo imeanza kupita na kupima maji kwa ajili ya kulinda wananchi wa Tanzania.

Aidha amefafanua Tume  hiyo ina majukumu makubwa matatu ikiwemo kudhibiti na kusimamia matumizi salama ya mionzi ili kulinda mazingira, wananchi wagonjwa pamoja na wafanyakazi dhidi ya matumizi ya mionzi.

Pili uhamasisha matumizi sahihi ya teknolojia ya mionzi au nyuklia katika sekta za afya, kilimo, viwanda, nishati, migodi na ujenzi.

Jukumu la tatu ni kufanya utafiti kuishauri serikali juu ya mikataba mbalimbali inayohusiana na mikataba ya nyuklia na kufanya kaguzi mbalimbali.

Amefafanua lengo kubwa ya kuja katika maonesho ya Sababasa ili kuweza kuendelea kutoa elimu kwa watanzania wawe na uelewa wa mionzi na kazi za Tume za Atomiki.

“Tunawakaribisha wananchi wote wa jiji Dar es Salaam na viunga vyake kufika katika banda letu waweze kujifunza na kupata elimu na uelewa na kazi zinazofanywa na  tume ” amesema

Afisa Utafiti kutoka TAEC Lazaro Meza amesema upimaji huo wa maji umetokana na sheria ya nguvu za atomu ya mwaka 2003 No.7 ya upimaji wa sampuli ya vyakula baada ya kufanyiwa mapitio sasa imekuja kupima vyakula pamoja na  maji kwa kuwa ni maji ni sehemu ya mapishi.

Amesema maji ni kiungo muhimu yakipata uchafuzi wa mionzi hivyo na chakula kitakuwa tayari kimepata madhara itokanayo na mionzi hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni