Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wanakuja na mtaala kuwapa ujuzi wanaofanya kazi shughuli za majumbani kuwahudumia wazee na watoto ili waweze kupata elimu zaidi na kupata vyeti watambulike pindi wanapoomba ajira ndani na nje ya nchi.
Hayo yameelezwa na Antony Kasore Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 yaTantrade katika banda hilo.
Amesema lengo la kuanzisha mtaala huo ili waweze kupata ujuzi wa kuhudumia makundi hayo likiwemo wazee, watoto na walemavu pamoja na kuweza kuwafanya watambulike kwa kupata vyeti kwa wale wenye uhitaji wa kwenda kufanya kazi nje ya nchi.
“Tumeona kuna wimbi la watanzania wengi kutafuta ajira za aina hiyo kuwa na uhitaji hivyo wakipata elimu na ujuzi itawasaidia katka shughuli zao na kutambulika” amefafanua
Mbali na mtaala huo pia wanakuja na mtaala wa utengenezaji wa vifaa tiba mbalimbali ambao ulikuwa haupatikani VETA na sasa umeanza katika vyuo viwili mkoani Musoma na Geita.
Ikiwemo kozi za kuwaanda watu wanaokwenda kufanya kazi viwandani kutengeneza mitambo, komputa kwaajili ya kuendesha na kurekebisha mitambo kozi tayari imeanza Desemba mwaka jana.
Amesema kozi hiyo imeanzishwa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza wawekezaji hasa katika eneo la viwanda hivyo watahitajika watendaji VETA inakuja kuandaa wataalamu hao ili waweze kujikomboa katika ajira hizo.
Vilevile amesema VETA kuna kozi za watu wa makundi maalum ikiwemo, wasioona, viziwi, walemavu na wengine ili waweze kupata ujuzi na kuendesha maisha yao.
Aidha Serikali imeongeza vyuo vya ufundi stadi kutoka vyuo 29 na kufika vyuo 80 ili watanzania wote waweze kunufaika na elimu ya ufundi stadi popote walipo.
Kasore amesema serikali inaenda kujenga vyuo 65 wilaya zote hivyo vitaenda kuwapa ujuzi watanzania kumfikia kila mmoja na shughuli zake aongeze ujuzi na ajira katika kila sekta ikiwemo,kilimo, afya, na nyingine na kufikia idadi ya vyuo 145 nchi nzima




0 Maoni